Luis Suarez akijipinda kuifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya tisa katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Espanyol
kwenye mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Kombe la Mfalme, maarufu
kama Copa del Rey usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou. Bao la pili
lilifungwa na Lionel Messi dakika ya 25 katika mchezo huo ambao mchezaji
mpya aliyesajiliwa kutioka Liverpool, Philippe Coutinho alicheza kwa
mara ya kwanza baada ya kuingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Iniesta dakika ya 68.
Barca inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza
Barca inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza

0 comments:
Post a Comment