Thursday, January 18, 2018

Theo Walcott ajiunga na EvertonEverton imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot katika mkataba ulio na thamani ya £20m katika kandarasi ya miaka mitatu na nusu.
Walcott, 28, ni mchezaji wa pili kusajiliwa na mkufunzi wa Everton Sam Allardyce katika dirisha la uhamisho la Januari baada ya mshambuliaji Cenk Tosun aliyesajiliwa kwa dau la £27m kutoka Besiktas.
Hatua hiyo inakamilisha huduma za Walcot za miaka 12 katika klabu hiyo ambapo alifunga magoli 108 katika mechi 397
"Kuna kitu muhimu kuhusu uhamisho huu najihisi vyema sana'', alisema
Klabu ya zamani ya Walcott Southampton pia walikuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo.
Lakini Walcott, ambaye hajaanza mechi yoyote ya ligi ya Arsenal msimu huu anaamini kwamba Allardyce anaweza kuimarisha mchezo wake.
''Nilihisi kwamba ni wakati nilifaa kuondoka'', alisema.
Ni uchungu lakini ni vyema na nataka kuimarisha mchezo wangu na kuisaidia Everton kushinda mataji kama ilivyokuwa awali.
Aliongezea: Mkufunzi amekasirika lakini hiki ndicho nilichotaka.
''Nilizungumza naye na nilihisi hasira aliyokuwa nayo na kile alichotaka kutoka kwangu''.
Katika taarifa yake , Arsenal ilisema: Sote tunamshukuru Walcott kwa mchango wake kwa Arsenal na tunamtakia kila la kheri.

0 comments:

Post a Comment