Orodha ya wachezaji wanaomiliko ndege za gharama duniani
imetoka, kama ambavyo wengi walitarajia CR7 anaongoza orodha ya
wachezaji wenye ndege za gharama kubwa duniani.

Cristiano
Ronaldo. Cr 7 yuko juu kabisa katika orodha hii kwani achilia mbali na
Ferrari na Galardo anazotumia bali Ronaldo ndio mwanasoka anamiliki
ndege ya gharama duniani ni Gulfstream G650 inayouzwa £31.7m.

Lioneil
Messi. Upinzani wa Cr7 na Lioneil Messi unaonekana sio uwanjani tu bali
sasa hata nje ya uwanja kwani baada ya CR7 anayefuatia ni Lioneil Messi
ambaye ana Embraer Legacy 650 yenye thamani ya £28.3m.

Zlatan
Ibrahimovich. Kwa sasa ni majeruhi ndani ya Manchester United lakini
maisha ya PSG, Barca, Intermilan na kwingineko yametosha kumfanya
kuchuna mpunga wa kununulia Citation Longitude yenye thamani ya £23.8m.

David
Beckham. Bado yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaodaiwa kuweka pesa
nyingi sana bani na Beckham kwake haikuwa shida kwenda kuitafuta
Bombadier Challenger 350 iliyomgharimu 21.5m

Paul
Pogba. Mchezaji ambaye amewahi kushikilia rekodi ya usajili ghali
wakati akitoka Juve kwenda Manchester United, Gulfstream G280 ndio ndege
anamiliki Pogba na ilimgharimu £20.4m.

Wayne
Rooney. Aliuzwa na United kwenda Everton katika dirisha lililopita la
usajili lakini kipesa bado yuko vizuri, Rooney anatumia Dassault Falcon
900LX ambayo thamani yake £15.8m.
Neymar. Kati ya wachezaji ambao wanapenda sana anasa ni Neymar,
hakuwa anapewa pesa nyingi sana lakini kama kawaida ya Wabrazil hawana
masihara yakija masuala ya matumizi, Neymar ana Embraer Legacy 450
ambayo thamani yake ni £12.2m.

Gareth
Bale. Raia wa Wales huyu ambaye majeraha yamemfanya asifurahie soka
siku za karibuni lakimi Bale anamiliki Cessna Citation XL Plus ambayo
thamani yake ni £9.7m.

Kaka.
Ricardo Kaka pamoja na kuwa mchezani anayelipwa sana lakini pia Kaka ni
kati ya wanasoka ambao wanatokea kwenye maisha mazuri, Kaka ambaye kwa
sasa amestaafu soka ana Cessna Citation Cj3 Plus ambayo thamani yake ni
£6.4m.

Ronaldinho.
Akiwa ametoka kutangaza kustaafu soka hivi majuzi tu lakini Gaucho yupo
nafasi ya 10 katika wanasoka ambao wanamiliki ndege za gharama, Dinho
ana Embraer Phenom ambayo aliinunua £2.9m.
0 comments:
Post a Comment