Tottenham kufanya walichowafanya United miaka 52 iliyopita leo?
Hii leo inaweza kuwa kipimo cha kwanza kikubwa kwa Alexis Sanchez tangu ajiunge na Manchester United ambapo hii leo watakwenda hadi uwanja wa Wembley kuwakabili Tottenham Hotspur.
Lakini Tottenham anwapokea United akiwa na rekodi chafu ya kupoteza michezo 80 mbele ya United rekodi ambayo inaweza kuwapa United kujiamini na kuwanyong’onyesha Tottenham hii leo.
Katika michezo 33 iliyopita ni mechi 4 tu ambazo Tottenham waliifunga Manchester United na wakaambulia kipigo mara 21 na kufanikiwa kupata suluhu 8 mbele ya mashetani hao wa Old Traford.
Wakati Tottenham walipokuwa katika uwanja wao wa White Hart Lane walifanikiwa kuifunga United katika michezo miwili mfululizo na mara ya mwisho kwa Tot kuipiga United mara 3 mfululizo ilikuwa miaka 1965/1966(52 iliyopita).
Michezo 6 iliyopita ambayo Manchester United wamecheza ugenini waliacha alama 2 tu na kubeba 16 na kwa ujumla katika michezo yao 8 iliyopita katika ligi ya EPL hawajawahi kuacha alama 3 katika mechi moja.
Lakini kwa upande wa Tottenham Hotspur tangu wapoteze mchezo wao dhidi ya Chelsea katika dimba lao la nyumbani mwezi August, hawajawahi kupoteza tena nyumbani kwao na sasa wana mechi 11 hawajawahi kupigwa Wembley.
Maurcio Pochettino anaonekana kushindwa kabisa kuwakabili timu kubwa EPL kwani mechi 5 vs United, City, Arsenal, Liverpool na Chelsea ameambulia alama 3 tu lakini rekodi yao siku za usoni katika uwanja wa nyumbani inawapa moyo kufanya jambo hii leo.
0 comments:
Post a Comment