Victor Valdes atundika daluga na mitandao ya kijamii
Aliichezea Barcelona michezo 387 na kushinda La Liga mara sita, Champions League mara tatu na Copa Del Rey mara mbili, huyo ni Victor Valdes ambaye sasa ameamua kutundika daluga zake.
Valdes ambaye amewahi kupitia katika klabu ya Manchester United anasema kwa sasa ameamua kuwekeza nguvu na akili zake kwa ajili ya kuisaidia familia yake na mambo.ya soka sasa baasi.
Valdes ambaye amewahi pia kushinda michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 akiwa na timu ya taifa ya Hispania huku pia akifanikiwa kushinda michuano ya mataifa ya Euro mnamo mwaka 2012.
Mwaka 2015 Victor Valdes aliahidi kwamba siku zake za kucheza mpira zikiisha atafuta account zake za mitandao ya kijamii jambo ambalo anaonekana kweli amelitimiza baada ya kuondoa account zake.
Taarifa zinadai baadhi ya timu zilikuwa bado zinataka kumpa nafasi Valdes lakini alikataa akisisitiza kwamba muda wake wa kucheza umekwisha na kisha kuwaaga mashabiki mtandaoni na kuzifuta account zake.
0 comments:
Post a Comment