Konta ameyasema hayo kufuatia kuingia katika mashindano matatu kwa mpigo ambayo ni Nottingham Open, Birmingham Classic na Eastbourne International yatakayo muwezesha kuwafiti wakati wa michuano ya
Wimbledon.
Johanna Konta mwenye umri wa miaka 26, mwaka jana alishindwa kufanya vizuri katika michuano hiyo ya Nottingham Open hata hivyo alifanikiwa kuwa mwanadada wa kwanza wa Uingereza kufika hatua ya nusu fainali ya Wimbledon kwa mchezaji mmoja mmoja tangu alivyoweza kufanya hivyo Virginia Wade mwaka1979.
“Huu ni moja kati ya msimu niupendao na hakuna wa kuufananisha hasa mashindano yakiwa nyumbani ambapo kuna mashabiki, marafiki na familia ikiwa nyuma yako inakushabikia,”amesema Konta kupitia chombo cha habari cha Skysport.
0 comments:
Post a Comment