Kenya inamsaka mkufunzi mpya wa timu yake ya taifa baada ya kocha Paul Put kujiuzulu miezi mitatu baada ya kuzinduliwa.
Hii
ilithibitishwa Jumatatu jioni na taarifa iliotolewa na shirikisho la
soka nchini humo FKF kupitia meneja wa mawasiliano na uhusiano mwema
Barry Otieno ambaye alielezea kwamba mkufunzi huyo alijiuzulu kutokana
na matatizo ya kibinafsi huku Stanley Okumbi akichukua mahala pake kwa
muda.''Shirikisho la soka la Football Kenya lingependa kuwaambia mashabiki wa soka nchini Kenya kwamba bwana Pual Put amejiuzulu rasmi kama mkufunzi wa timu ya taifa kutokana na maswala ya kibinafsi.
''Hatahivyo kujiuzulu kwa kocha huyo ni pigo katika harakati za timu ya taifa kuelekea katika kufuzu mashindano ya AFCON 2019 kwa kuwa alikuwa kiungo muhimu cha timu''.
- Timu ya Kenya Harambee Stars yapata kocha mpya
- Wenyeji Kenya wafuzu kwa fainali Cecafa
- Zanzibar sasa yaomba kutambuliwa na Fifa
- Zanzibar: Hatuogopi Kenya hata kama wako nyumbani
''Mwisho FKF inamshukuru bwana Put kwa huduma zake wakati akiwa mkufunzi mkuu wa Harambee Stars mbali na kumtakia mema katika kazi yake siku zijazo'', taarifa hiyo ilisema.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.