Msuva alikuwa sehemu ya kikosi cha Difaa El Jadida kilichocheza dhidi ya Sport Bissau E Benfica na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 10-0, kwa upande wa Msuva amefanikiwa kufunga hat-trick katika game hiyo na kuhusika katika upatikanaji wa magoli matatu mengine akitoa pasi mbili za magoli na akisababisha penati.
Hii ndio inakuwa hat-trick ya kwanza ya Simon Msuva kufunga akiwa na Difaa El Jadid, magoli mengine ya Difaa El Jadid yalifungwa na Ahadad aliyefunga magoli matano, N’diaye na Bilal El Megri, sasa Difaa El Jadida watakuwa na kazi nyepesi katika mchezo wa marudiano kwani watakuwa wanahitaji sare tu au hata wakipoteza kwa idadi ya magoli 9-0 watakuwa wamefuzu.
0 comments:
Post a Comment