Klabu ya Manchester
City imekubali mkataba wa kumsajili kiungo wa kati wa Shakhtar
Donetsk's 24 na raia wa Brazil Fred kwa dau la £44.5m mwisho wa msimu
huu. (Goal)
Klabu za Manchester City na Manchester United zina hamu kumsajili beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire, 24. (Mirror)
Chelsea huenda ikamuajiri mkufunzi wa zamani wa Hull na Watford Marco Silva kusimamia klabu hiyo kwa muda mfupi iwapo watamfuta kazi Antonio Conte kabla ya mwisho wa msimu huu.. (Times - subscription required)

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 25, hajapinga uhamisho kurudi katika klabu yake ya zamani Real Madrid. Alipoulizwa iwapo anaweza kurudi Real Madrid alisema kuwa anafurahia kusalia na Blues lakini akaongezea kuwa ''Madrid ni Madrid''.(Mail)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane ametaja kuwa habari za uongo kuhusu ripoti kwamba klabu hiyo inapanga kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania ,25 Isco. (El Pais - in Spanish)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 26, huenda akabaini kwamba kazi yake katika klabu hiyo imekwisha kufuatia kuwasili kwa aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Dortmund-Emerick Aubameyang, 28, kulingana na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Emmanuel Petit. (sun)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema kuwa mkufunzi wa Everton Sam Allardyce alichelewa kuomba msamaha kwa kumkejeli anavyozungumza.. (Times - subscription required)

Wamiliki wa klabu ya Swansea wanasema kuwa rekodi yao katika soko la uhamisho imechanganyika na dirisha la uhamisho la msimu huu lilikuwa baya zaidi. (Guardian)

Mshambuliaji wa Manchester United striker Marcus Rashford, 20 ana mali yenye thamani ya £2m kufikia mnamo Aprili 2017 ikilinganishwa na £100 mwaka mmoja uliopita. (Sun)Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney anasema kuwa angependelea siku moja kuwa mkufunzi katika ligi ya Uingereza.. (Telegraph)

0 comments:
Post a Comment