Tayari umri unamtupa mkono Cr7 na migui yake imeshaanza kuonekana kuchoka, wengi wanaamini muda wa Cristiano Ronaldo kuwa bora umekwisha na sasa ni wakati wa vijana wengine kuvaa viatu vyake.
Cristiano Ronaldo mwenyewe amekiri kwamba kwa sasa hawezi kufanya yale aliyoyafanya akiwa na miaka 20, kauli ambayo inaonesha hata yeye mwenyewe ameshaanza kukubali kwamba uwezo wake umekwisha.
Xavi anaamini kwa sasa kama mmoja kati ya Ronaldo na Messi ataondoka katika ufalme wake wa soka baasi moja kwa moja itakuwa nafasi ya mshambuliaji wa PSG Neymar kuchukua nafasi ya kuwa bora duniani.
Ukiacha Neymar, Xavi anaamini Kylian Mbappe yuko katika nafasi nzuri kushindana na Neymar kugombea tuzo hiyo na hii inamaanisha kuna uwezekano mkubwa PSG wakatoa washindani wawili wa Ballon D’Or siku za usoni.
0 comments:
Post a Comment