Simba
ilipata penati mnamo dakika ya 80 kwa John Bocco kuchezewa madhambi na
Mwamuzi wa mchezo kuamuru penati hiyo ipigwe kuelekea lango la Prisons.
Manara
amewaita ni wanafiki huku akieleza kuwa kuwa wamekuwa wakiiandama Simba
kila siku pale inapotokea inastahili kupewa haki yake Uwanjani.
Mkuu
huyo wa kitengo ameeleza baadhi ya wadau na wale wote waliopinga penati
hiyo, wamekuwa wakiisema Simba vibaya pale inapotokea imefanyiwa sivyo
Uwanjani na badala yake wanashindwa kuitetea.
Simba
iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mcheo huo uliopigwa Uwanja wa
Taifa huku magoli yakifungwa na Bocco pamoja Emmanuel Okwi.

0 comments:
Post a Comment