Mmiliki wa Fulham, Jacksonville Jaguars, amtuma ofa katika Chama cha Soka cha England (FA) akitaka kuununua Uwanja wa Wembely uliopo London.
FA wamethibitisha kupokea ofa hiyo kutoka kwa mmiliki wa klabu ya Fulham na NFL inayosema atatoa kiasi cha pauni milioni 300 kwa FA na 500 kwa ajili ya Uwanja.
Kwa mujibu wa Jaguars, amesema kuwa dhumuni na malengo ya kutaka kuununua Uwanja huo ni kutaka kuusaidia na kuukuza zaidi mchezo wa soka ambao ni ajira.
Kamati ya FA iliketi jana Alhamis kuzungumzia ofa hiyo ambayo imetumwa na mmiliki huyo wa Fulham.
Uwanja wa Wembley una uwezo wa kuingiza zaidi ya mashabiki 90,000 baada ya kufunguliwa rasmi mwaka 2007.
0 comments:
Post a Comment