Monday, May 21, 2018


Pamoja na uwekezaji mkubwa wa zaidi ya £160m lakini kipigo cha bao moja kwa nunge kutoka kwa Chelsea katika fainali ya FA hapo jana kimewafanya United kumaliza msimu wa 2017/2018 bila kombe.
Pamoja na kwamba hii ni mara ya kwanza kwa Mourinho kucheza misimu miwili ya ligi bila kikombe cha ligi, lakini hii ni mara ya nne kwa Mreno huyu kucheza msimu mzima bila kutoka na kikombe chochote.
Tangu Jose Mourinho awe mwalimu wa Fc Porto mwaka 2002, ni mwaka 2007/2008, 2013/2014, 2015/216, na msimu huu ndio ambapo Mourinho alicheza msimu mzima bila kikombe cha aina yoyote.
Ushindi wa jana wa Chelsea sasa unafanya kikombe cha FA kwenda mara 11 katika misimu 17 iliyopita, ni Arsenal ndio timu inaongoza kubeba kombe hilo kutoka London(6) huku Chelsea akibeba mara 5.
Ushindi huo wa Chelsea umewafanya sasa kuwahi kubeba kombe hilo mara 8 katika historia na kuwafanya kuwa nafasi ya 3 kwenye timu zilizobeba kombe hilo mara nyingi, wa kwanza ni Arsenal(13) kisha United(12).

0 comments:

Post a Comment