Friday, May 4, 2018

HATUA ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika inaanza leo kwa mechi tatu kucheza nchi za Botswana, Misri na Algeria. 
Nchini Botswana, wenyeji Township Rollers watawakaribisha KCCA ya Uganda Uwanja wa Taifa mjini Gaborone kuanzia Saa 1: 00 usiku, wakati nchini Misri wenyeji Al Ahly watawakaribisha ES Tunis ya Tunisia Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria kuanzia Saa 4:00 usiku katika mchezo za Kundi A na Algeria wenyeji, MC Alger watakuwa wenyeji wa Difaa Hassan El- Jadida ya Morocco kuanzia Saa 4:00 katika mchezo wa Kundi B.
Aliyekuwa kocha wa Yanga SC ya Tanzania, George Lwandamina kesho ataanza rasmi kazi kwa mwajiri wake mpya, Zesco United ikimenyana na Mbabane Swallows ya Swaziland kuanzia Saa 10: 00 jioni Uwanja wa Ndola, Zambia.
Lwandamina ameondoka Yanga mwezi uliopita baada ya kuiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na kurejea timu yake ya zamani, Zesco.            

George Lwandamina kesho ataanza rasmi Zesco United ikimenyana na Mbabane Swallows ya Swaziland 

RATIBA KAMILI MECHI ZA UFUNGUZI LIGI NYA MABINGWA
KUNDI A
Mei 4, 2018;  Ahly (Misri) vs Esperance (Tunisia) Saa 4:00 usiku Alexandriua           
Mei 4, 2018; Township Rollers (Botswana) vs KCCA (Uganda) Saa 1:00 usiku Gaborone           
KUNDI B
Mei 4, 2018; MC Alger (Algeria) vs Difaa El Jadidi (Morocco) Saa 4: 00 usiku Algiers           
Mei 5, 2018; TP Mazembe (DR Congo) vs ES Setif (Algeria) Saa 10: 00 jioni Lubumbashi   
KUNDI C
Mei 5, 2018; AS Port (Togo) vs Horoya (Guinea) Saa 1:00 usiku Lome             
Mei 5, 2018; Sundowns (South Africa) vs Wydad (Morocco) Saa 3: 00 usikumPretoria         
KUNDI D;
Mei 5, 2018; Zesco (Zambia) vs Swallows (Swaziland)Saa 10: 00 jioni Ndola            
Mei 5, 2018; Primeiro Agosto (Angola) vs Etoile (Tunisia) Saa 1:00 usiku Luanda

0 comments:

Post a Comment