Friday, May 4, 2018


Mshambuliaji Diego Costa akiinua mkono wake juu kushangilia baada ya kuifungia bao pekee Atletico Madrid dakika ya 45 na ushei katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal usiku wa Alhamisi Uwanja wa Wanda Metropolitano mjini Madrid, Hispania katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Europa League. Atletico inaingia fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza London wiki iliyopita na itamenyana na Olympique Marseille iliyoitoa Red Bull Salzburg ya Austria kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-0 Ufaransa na kufungwa 2-1 ndani ya dakika 120 Wals-Siezenheim

0 comments:

Post a Comment