Kiungo
mkabaji wa Simba, Jonas Mkude amefanikiwa kuandika rekodi ya pekee
klabuni hapo baada ya juzi Alhamisi timu hiyo kutangaza kuwa mabingwa
wapya wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Simba
ilitangaza kuwa mabingwa wapya ligi kuu msimu huu baada ya Yanga
iliyokuwa ikichuana na timu hiyo kuwania ubingwa huo kufungwa na Prisons
mabao 2-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliyofanyika kwenye Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
Rekodi
hiyo ya pekee ambayo Mkude ameiandika klabuni hapo ni ile ya kuwa
mchezaji pekee aliyefanikiwa kunyakua ubingwa wa pili wa ligi kuu akiwa
na timu hiyo bila ya kuhama ndani ya kikosi hicho.
Nyota
wengine waliochukua ubingwa mara mbili na klabu hiyo lakini wao
waliwahi kuhama kwa nyakati tofauti ni Mganda, Emmanuel Okwi, wazawa
Mwinyi Kazimoto na Shomari Kapombe. Mara ya mwisho Simba ilikuwa
imechukua ubingwa msimu wa 2011/12.
Mkude
alisema kuwa: “Nimefurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa hilo kwani
nilipambana kwa muda mrefu kwa ajili ya mafanikio hayo lakini sasa ndoto
zangu zimetimia.
“Nawashukuru
sana viongozi wangu, wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki wote wa
Simba kwa ushirikiano mkubwa tuliokuwa nao msimu huu, nimuombe Mungu tu
aendelee kutujalia hali hii ya ushirikiano iendelee katika mechi zetu
zilizobakia lakini pia katika misimu mingine yote,” alisema Mkude.
CHANZO: CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment