Kikosi cha Simba kimeondoka jana jijini Dar es Salaam kuelekea Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United.
Simba ambao tayari ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameondoka wakiwa na rekodi ya kuutwaa ubingwa wa ligi bila kupoteza mchezo hata mmoja huku wakiwa na mechi tatu mkononi.
Kikosi hicho kilipitia Dodoma na kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya kuendelea na safari ya Singida kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa Mei 12 2018.
Simba wameandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuweka kambi ya muda mfupi Dodoma baada ya kupewa hadhi ya kuwa Jiji na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Joseph Magufuli siku kadhaa zilizopita.
Rais Magufuli alitangaza rasmi Dodoma kuwa jiji katika siku ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika Aprili 26 2018.
Kitendo cha Simba kupita Dodoma na kuweka kambi fupi jana kimeipa historia ya kuwa klabu ya kwanza inayoshiriki Ligi Kuu Bara kufanya hivyo ndani ya jiji hilo jipya lilipewa hadhi hiyo na Rais Magufuli.
0 comments:
Post a Comment