Friday, May 18, 2018



Mashabiki na wapenzi wa soka wengi duniani walishangazwa na kocha wa club ya Arsenal Arsene Wenger kutangaza maamuzi ya kuondoka club ya Arsenal baada ya msimu wa 2017/2018 kumalizika, hiyo inatokana na kocha huyo kudumu katika club hiyo kwa miaka 22.

Baada ya Wenger kutangaza kuwa anaondoka Arsenal na kudai kuwa ataendelea kuwa kocha wa mpira kama kawaida, wengi walikuwa na hamu ya kutaka kufahamu kocha Arsene Wenger ataenda timu gani atastaafu? huku wakisubiri siku atakayotoa hatma yake.
Wenger mwenye umri wa miaka 68 kwa sasa amesema kuwa atatangaza hatma ya kuwa anaenda club gani kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia, kwani amepokea ofa kadhaa na yeye nbado yupo katika mshituko kufuatia maamuzi aliyoyanya ya kuondoka Arsenal.

“Bado mapema kutangaza nitaenda wapi bado sijasafisha hata desk langu Arsenal na bado nipo katika mshituko najipa muda mpaka June 14 kabla ya kuanza Kombe la Dunia kuamua pakwenda, najua swali nitaendelea kufundisha soka? au ni muda wa kufanya kazi nyingine? Jibu ninaloweza kutoa kwa sasa ni kuwa nitaendelea kufanya kazi”>>> Wenger
Wenger baada ya kudumu katika club ya Arsenal kama kocha mkuu aliiongoza kwa mara ya mwisho wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Huddersfield Town uliyomalizika kwa Arsenal kupata ushindi wa goli  1-0.

0 comments:

Post a Comment