Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low amewashitua wapenzi wa soka baada ya kumtoa kwenye kikosi cha wachezaji 23 Winga hatari wa Manchester City, Leroy Sane hii leo ikiwa ni harakati za kujiweka sawa kuelekea michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi.
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter Shirikisho la soka la Ujerumani limethibitisha kuachana na mchezaji huyo mchanga zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mtanange wa kombe la Dunia kuanza nchini Urusi.
Winga hatari wa Manchester City, Leroy Sane
Mapema mwaka huu, Sane ametwaa tuzo ya mchezaji mdogo wa kulipwa wa mwaka ligi kuu ya nchini Uingereza (PFA) akiwa anaitumikia klabu yake ya Manchester City.
Kikosi cha timu ya taifa ya Ujeruman
i
i
0 comments:
Post a Comment