Mabingwa
wa ligi kuu nchini Uingereza, Manchester City wapo kwenye vita kubwa na
klabu ya Everton dhidi ya kuwania saini ya kijana mwenye umri wa miaka
14, Omari Forson.
Forson
anayekipiga kwenye klabu ya Tottenham amekuwa kivutio kikbwa cha timu
hizo kutokana na uwezo aliyonao katika kufumania nyavu huku saini yake
ikihitajika kwa udi na uvumba kwenye dirisha hili la usajili.Manchester City na Everton zote zimeshaweka kitita cha fedha mezani kwaajili ya kijana, Omari Forson, picha akiwa na West Ham
Vyombo mbalimbali vya habari vimeanza kumwilika kipaji kikubwa alichojaaliwa Forson ambaye mwenye anandoto za kwenda kufanya mazoezi kwenye klabu ya Everton wiki hii.
Mshambuliaji
huyo anayetumia guu la kushoto katika kupachika mabao amekuwa ahihitaji
kwenye klabu ya City hata kabla hajaanza kuonekana kipaji alicho nacho
alipokuwa na miaka tisa mwaka 2014 alipokuwa West Ham.
Tottenham ilikwenda nyumbani kwa Forson ili kufuatilia maendeleo ya kijana huyo katika kuhakikisha hakuna anayeweza kumsajili.
Forson
ambaye wazazi wake ni raia wa Ghana wanao hishi Uingereza amekuwa na
mvuto mkubwa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na watu wengi kufuatilia
video zake zinazo muonyesha akitupia magoli.
0 comments:
Post a Comment