Monday, July 30, 2018


Staa wa soka wa club ya Paris Saint Germain ya  Ufaransa na timu ya taifa ya Brazil Neymar jina lake lilikuwa kwenye headlines sana wakati wa fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2018 zilizofanyika nchini Urusi kutokana na kitendo chake cha kudaiwa kujiangusha.
Neymar alikuwa anadaiwa kuwa anajiangusha sana wakati wa game za michezo hiyo, leo amenukuliwa na baadhi ya mitandao kuwa alikuwa anadanganya wakati mwingine wakati wa fainali za michuano hiyo ili kuonekana kama ameumizwa sana.
“Unaweza ukafikiria nadanganya na kweli wakati mwingine nadanganya lakini ukweli ni kwamba wakati mwingine unaumia uwanjani, unaweza ukahisi najiangusha sana muda wote”>>>Neymar

0 comments:

Post a Comment