Baada ya timu ya taifa ya Hispania kuondolewa katika michuano ya kombe la
dunia inayoendelea nchini Urusi, sasa walau Wahispania wamepata pa kujifichia na
cha kuzungumzia.
Ni Rafael Nadal, tangu mwaka 2011 Mhispania huyo hajawahi kuingia katika robo fainali ya michuano ya Wimbledon, Nadal amefanikiwa kufudhu kwa robo fainali baada ya kumshinda Jiri Vesely kwa seti 6-3, 6-3, 6-4.
Kwa
matokeo haya sasa Nadal anakwenda kukutana na kati ya Juan Martin Del Potro raia
wa Argentina ama Gilles Simon raia wa Ufaransa katika robo fainali ya michuano
hiyo.
Lakini habari kubwa baada ya Nadal kufudhu ni uwepo wa Rodger Federer kwenye michuano hiyo ambaye naye amefudhu kwa robo fainali baada ya kumchapa bila kupoteza seti Adrian Mannarino wa Ufaransa kwa seti 6-0, 7-5 na 6-4.
Mwaka
2008 wawili hawa walikutana katika hatua ya fainali na ndio fainali ambayo
wataalamu wa hizi mambo wanasema ndio fainali bora kabisa ya mchezo wa tennis
kuwahi kutokea na sasa inaonekana inaweza ikajirudia.
Kuanzia mwaka 2006 hadi 2011 Rafael Nadal alikuwa katika kiwango cha juu sana akifanikiwa kutinga fainali mara 5, lakini kuanzia 2011 alianza kuibuka kapa katika Wimbledon na majeruhi aliyopata 2009 yakitajwa kama chanzo cha kumshusha.
Hadi
sasa Federer ameshashinda kwa seti 32 mfululizo na hii ina maanisha yuko nyuma
ya seti 5 ya Nadal ambaye ameshinda seti 37 mfululizo, lakini wote hawajaifikia
rekodi ya Bjorn Borg aliyewahi kushinda seti 41 mfululizo 1979-1981.
Ni Rafael Nadal, tangu mwaka 2011 Mhispania huyo hajawahi kuingia katika robo fainali ya michuano ya Wimbledon, Nadal amefanikiwa kufudhu kwa robo fainali baada ya kumshinda Jiri Vesely kwa seti 6-3, 6-3, 6-4.
Lakini habari kubwa baada ya Nadal kufudhu ni uwepo wa Rodger Federer kwenye michuano hiyo ambaye naye amefudhu kwa robo fainali baada ya kumchapa bila kupoteza seti Adrian Mannarino wa Ufaransa kwa seti 6-0, 7-5 na 6-4.
Kuanzia mwaka 2006 hadi 2011 Rafael Nadal alikuwa katika kiwango cha juu sana akifanikiwa kutinga fainali mara 5, lakini kuanzia 2011 alianza kuibuka kapa katika Wimbledon na majeruhi aliyopata 2009 yakitajwa kama chanzo cha kumshusha.
0 comments:
Post a Comment