EMMANUEL
Amunnike habari zake kwa sasa zimeshafungwa kwa kuwa amekubaliana na hali
halisi ya kukiacha kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania.
Matarajio ya
wengi ilikuwa ni kwenye michuano ya Afcon kufanya vema na mwisho wa siku kila
kitu kikawa tofauti na vile ambavyo wengi walikuwa wanaamini.
Ni jambo
jema hasa kwa kuwa hakuna mgogogro wowote na pande zote mbili zimekubalina hasa
ukizingatia kwamba watanzania wengi wanapenda kuona matokeo chanya hata TFF nao
hesabu zao ni kuona Taifa linapata matokeo chanya.
Rekodi
ambayo ameiweka itabaki kwenye kumbukumbu kwani licha ya kutimuliwa ni yeye ameiongoza
timu kutinga hatua ya makundi ya michuano mikubwa Afrika ya Afcon akiwa ni
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania.
Hii
imewezekana baada ya kupita miaka 39 ambayo wachezaji wote wanaoitumikia kwa
sasa timu ya Taifa hakuna hata mchezaji mmoja aliyekuwa anakipiga ndani ya
kikosi cha timu ya Taifa kwa wakati huo hivyo inamaanisha kwamba ni muda mrefu
umepita.
Mema
aliyoyafanya tutayakumbuka na hata maumivu ya kupoteza kwenye michuano yetu ya
Afcon haitafutika kwani ni rekodi na hatuwezi kukataa kwamba mechi zetu tatu
zote tulifungwa na tulimaliza kundi C tukiwa hatuna hata pointi moja zaidi ya
kubeba furushi la mabao nane nasi tukifunga mabao mawili.
Ni rekodi yenye
maumivu na uchungu hivyo inatoa taswirwa kwamba wakati ujao TFF ambao ndio
wanaochagua kocha wa kuinoa timu ya Taifa wanatakiwa kuwa makini na kusimamia
weledi wa kazi na sio kuweka mapenzi yao binafsi kwenye maslahi makubwa ya
nchi.
Tukumbuke kuwa
kwa sasa timu ya Taifa ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu Ettiene Ndayiragije akipeana sapoti na wazawa,
Suleman Matola na Juma Mgunda na mchakato uliopo kwa sasa ni kufuzu michuano ya
Chan.
Ukiachana na
Chan bado tunahitaji kuwa na kocha mkuu wa timu ya Taifa ambaye atasuka kikosi
kipya cha ushindani kwa ajili ya kufuzu pia michuano ya Afcon.
Hivyo bado
kuna uhitaji wa kumpata kocha mwenye uwezo na mwenye kiu ya mafanikio pale
ambapo anakuwa anafanya kazi na sio ilimradi tu.
Nasema hivyo
kwa sababu ya yale ambayo yamejitokeza kwa Amunike alikuwa ni mpole wa sura ila
mengi nyuma ya pazia wanayajua wachezaji wenyewe licha ya kutokusema hata TFF
nao wanajua namna alivyokuwa.
Mwalimu wa
aina hii kama atapewa nafasi tena basi kuyafikia mafanikio ya soka itakuwa ni
historia hivyo kwa hili TFF liwe darasa na maamuzi yao yawe yenye manufaa kwa
Taifa.
Ukubwa wa
timu ya Taifa uendane na ukubwa wa mwalimu atakayekuja kuifundisha timu, vigezo
muhimu vizingatiwe kwa kuifuatilia rekodi yake na kujua namna gani anaweza
kumudu mazingira yetu.
Namna pekee
ya kumpata kocha bora ni kufanya utafiti mzuri tena wa kina na kutumia jopo la
wataalamu kumchunguza huyo ambaye mnahitaji.
0 comments:
Post a Comment