Tuesday, July 30, 2019


 AGOSTI 6 kwa kuchezwa mechi ya kirafiki baina ya Wekundu hao dhidi ya Power Dynamo kutoka Zambia.

Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Crescentius Magori amesema kuelekea Tamasha hilo ambalo limedhaminiwa na SportPesa litaanza Julai 31 na itakuwa litaitwa "SportPesa Simba Wiki" 

Matukio yake yatakuwa kama namna hii:

Julai 31

Kikosi kitarejea kutoka kambini nchini Afrika na kusaini mkataba na wadhamini wa jezi na vifaa vya michezo.

Siku hiyo hiyo Saa 6 usiku kupitia mitandao yote ya kijamii ya klabu ya Simba itazindua jezi zake za nyumbani, ugenini na Neutral.

Agosti 1

Jezi za Simba zitaanza kuuzwa na
Kuzindua kadi ya za Wanachama za kielectroniki (Smart Card) kwa ajili ya kunua tiketi moja kwa moja.

Agosti 2

Tiketi za Platinum za shilingi 100,000 na zile za Platinum Plus za shilingi 150,000 zitaanza kuuzwa.

Agosti 3

Wachezaji wa Simba wataenda kutoa msaada katika Hospitali ya Ocean Road na shughuli hiyo itafanywa na Wana Simba wote nchi nzima.

Kutazinduliwa wimbo maalum wa klabu ya Simba ambao utakuwa rasmi na kwa wale walionunua tiketi za Platinum na Platinum Plus watapiga picha na wachezaji wa Simba wakiwa na familia zao kuanzia saa 4 asubuhi.(Photo Shots)

Baada ya zoezi la kupiga picha wachezaji wataenda kutembelea watoto Yatima sehemu mbalimbali Dar es Salaam.

Kuwasili kwa timu ya Power Dynamo.

Agosti 5

1.Pre Match Meeting

2. Mkutano wa Waandishi wa Habari, makocha na manahodha wa timu zote wataongea.

Agosti 6 
Kilele cha Simba Day

1. Burudani mbalimbali kuanzia saa 4 asubuhi

2. Mechi ya Simba Queens saa 8

3. Mechi ya Simba U20 vs Faountain Gate Academy saa 9

4. Utambulisho wa wachezaji 
5. Mechi kati ya Simba dhidi ya Power Dynamo

Agosti 7

Chakula cha mchana kati Simba na Wageni wao Power Dynamo.

Katika kilele cha tamasha hilo kauli mbiu itakuwa Iga Ufe This is Next Level 10 years Anniversary of Simba Week.

0 comments:

Post a Comment