Gareth Bale
amejiondoa katika safari ya Real Madrid ya kwenda Munich kwa ajili
ya shindano la kabla ya msimu kufuatia hatua yake ya pendekezo lake la
kuhamia Uchina ambalo halikufanikiwa.
Inafahamika kwamba Bale
hayuko vizuri kiakili kucheza baada ya rais wa Real Florentino Perez
kumzuwia kujiunga na klabu ya Jiangsu Suning ya Uchina.- Mwandishi wa habari Tanzania ''akamatwa''
- Ni nani anayefaidika na ushirikiano wa Beyoncé na wasanii wa Afrika?
- Uchumi wa Tanzania waanza 2019 kwa kuyumba
- Mwili wapatikana nyumbani kwa nyota wa Arsenal
Zidane aliongeza kuwa kutoka kwake kwenye katika Real lingekuwa ni jambo ambalo ni " bora kwa kila mmoja ".
Real ambao ni washindi wa ligi ya Uhispania mara 33-watacheza na klabu aliyoichezea zamani ya Bale-Tottenham Jumanne katika mechi ya ufunguzi wa mashindano yatakayozijumuisha Bayern Munich na Fenerbahce.
Kiungo wa nyuma-kushoto Danny Rose amejumuishwa katika kikosi cha Spurs , licha ya kuachwa kwenye safari ya michuano ya kabla ya msimu barani Asia ili atafute klabu mpya.
Bale alijiunga na klabu hiyo ya Uhispania kwa malipo ya pauni milioni 85 alitokea klabu ya Tottenham mnamo mwaka 2013 katika mkataba uliokuwa mkubwa zaidi duniani wakati huo.
Amebakiza miaka mitatu ya mkataba wake na klabu ya Bernabeu ambako alishinda vikombe vinne vya Championi Ligi, moja taji la La Liga title, Copa del Rey, la tatu Uefa Super Cups na klabu tatu katika kombe la dunia.
Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Wales aliifungia Real mabao matatu, pamoja na mkwaju wa penati katika fainali nne za Championi Ligi waliposhinda mashindano hayo mwaka 2014, 2016, 2017 na 2018.
Hata hivyo , matatizo ya majeraha yalimfanya acheze michezo 79 tu ya mwanzo ya La Liga katika misimu minne iliyopita.
Aliichezea Real Madrid mechi 42msimu uliopita lakini alizomewa na baadhi ya mashabiki wakati mwingine wakati wa mechi.
Imekuwa ikiripotiwa kuwa Real ilizuwia kuhama kwa Bale kwasababu walikuwa wakidai gharama ya uhamisho wake.
- Zidane: Gareth Bale 'anakaribia' kuondoka
- Gareth Bale kurejea uwanjani leo
- Real Madrid yasitisha uhamisho wa Gareth Bale
"Jitokeze Gareth, fanya mahojiano , ongea," alisema John Toshack mwenye umri wa miaka 70 . "umekuwa hapa kwa miaka sita au saba sasa . Huongei lugha ya wenyeji. Hilo ni tusi kwa watu unaowafanyia kazi.
"Mambo haya kwenda vizuri hapa Uhispania, na inanisikitisha.
"Amekuwa muhimu katika Real Madrid. Ni jambo la huruma sana kwamba hakuwahi kujihusisha zaidi kidogo na nchi ambamo anaishi na mashabiki ambao wako pale kila wiki.
"Gareth, njoo. Chukua muda kidogo na ujifunze lugha."
0 comments:
Post a Comment