Wednesday, July 25, 2018



Klabu ya Arsenal imekanusha taarifa zinazozagaa mitandaoni kwamba mkurugenzi wake Ivan Gazidis anatarajia kujiunga na miamba ya Ac Milan
Raisi wa chama cha soka cha Uturuki Mh. Yildirim Demiroren amempongeza Mesut Ozil kwa uamuzi aliochukua wa kujiuzulu kuitmikia timu hiyo ya taifa. Hata hivyo raisi wa nchi hiyo pia ameungana na Ozil katika harakati za kupinga ubaguzi wa kidini na rangi.
Stoke city wamemsajili Tom Ince, kutoka Huddersfield town kwa ada ya uhamisho wa awali wa paundi million 10, ambayo inaweza kupanda mpaka million 12

Winga huyo, mwenye umri wa miaka 26, amesaini mkataba wa miaka minne. Fulham wamemsajili Kipa kutoka Besiktas, Fabri kwa mkataba wa miaka Mitatu. Fabri mwenye umri wa miaka 30, alifanya kaz na Kipa wa Fulham, Jose Sambade Carreira katika klabu ya Deportivo La Coruna
Klabu ya Borrusia Dortmund, imefikia makubaliano ya kuumuza winga wao Andrei Schrulle, kujiunga na klabu ya Fulham. Schrulle, atasafiri leo kuelekea London, kufanyiwa vipimo na kujiunga na klabu hiyo. Schrulle, ameichezea Chelsea michezo 44 na kufunga mabao 11 Mwaka 2015 kabla ajaondoka klabu ya Chelsea.
Klabu ya Biashiara United, imekamilisha usajili wa wachezaji wanne ikiwa ni maboresho ya kikosi chao kwa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara. Wachezaji hao ni Lambele Jerome kutoka Lipuli FC, Yohana Moris, kutoka Mbeya City Frank Sekule, kutoka Dodoma FC, na Daniel Manyenye, kutoka Toto FC.
Klabu ya Real Madrid yakubaliana binafsi na Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois, lakin wataendelea kumuangalia Hugo Lloris endapo uhamisho wa Courtois ukishindikana
Gelson Martin, amejiunga na klabu ya Athletico Madrid, kwa mkataba wa miaka 6.

0 comments:

Post a Comment