Wednesday, July 25, 2018


“Nimezaliwa na kukulia Ujerumani, kwanini watu hawaniheshimu kama mjerumani mwenzao”Ozil
Özil ana asili ya Turkish-German [Uturuki na Ujeruman]. Hajawahi kukana asilia yake, wala haoni aibu kusifia asilia yake.
Aliwahi kunukuliwa akisema “Kipaji changu ni moja ya lulu ya kituruki, nina nidhamu kama walivyo waturki wote, jitiahada zangu zote nimezilekeza Ujerumani”

Licha ya kuwa na asilia ya Uturuki lakini maisha yake yote ameyawekeza ndani ya Ujerumani. Uzao wa Özi unatokana na kabila la Devrek, Zonguldakin linalopatikana nyanda za kaskazini magharibi mwa Uturuki.
Özil ni Muislam safi. Anafunga mwezi mtukufu wa Ramadan na mara kadhaa amekuwa akihudhuria safari za kuhiji Mecca. Hata hivyo kutokana na kazi Özil anakiri kwamba amekuwa hafuaati vyema mfungo.
Mwaka 2010, Özil alipewa tuzo za Bambi baada ya kuonekana kwamba yeye alikuwa raia ambaye siye mzawa wa Ujerumani lakini aliweza kumudu tamaduni za taifa hilo bila shida yeyote. Hii tuzo ilikuwa maalumu kwake kutokana na uvumilivu wake.
Özil pia amemuoa Miss Turkey, Amine Gülşe. Bila shaka Ozil alikuwa na mapenzi ya dhati kutoka moyoni.
Shida ni timu yake ya taifa ya Ujerumani. Hivi majuzi Leroy Sane alitoswa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa. Wapo waliosema amebaguliwa kwa kuwa ni mweusi. Ndio inawezekana kabisa.

Wajerumani ni wabaguzi sana hasa kwa ngozi nyeusi.
Ujerumani haijawahi kuwa na mchezaji mweusi kwenye timu yao kuanzia mwaka 2002 kurudi nyuma kwenye kikosi chao cha kombe la dunia. Kuna mwanaume mmoja tu anaitwa Gerald Asamoah ndiye aliyevunja mwiko wa Wajerumani na kuwa mchezaji wa kwanza kuitwa kwenye kikosi chao cha kombe la dunia mwaka 2002.
Mwandishi nguli JOSH SIPPIE anasema Asamoah hakuwa mzaliwa wa Ujerumani kwani alihamia taifa hilo mwaka 1989 akiwa na miaka 10 tu lakini aliwakonga nyoyo. Hapo awali mchezaji wa Borussia Dortmund Erwin Kostedde, mtoto wa mwanajeshi wa kimarekani aliyekuwa mweusi mwaka 1974 alipata bahati ya kuitwa timu ya taifa lakini alicheza michezo mitatu tu wala hakufanikiwa kwenda na timu ya taifa kule Mexico 1974.

Jimmy Hartwig, mtoto mwingine wa mwanajeshi wa kimarekani aloyekuwa na ngozi nyeusi nae alibaguliwa sana 1979 alipokuwa akiichezea Hamburg na hakufanikiwa kucheza kombe la dunia 1978.
Baada ya Assamoah, watu kama Cacau, Boateng na Rudiger ni wachezaji waliofanikiwa kuitwa timu ya taifa. Lakini haijawahi kutokea Ujerumani ikawa na wachezaji weusi watatu kwenye kikosi chao. Ilikuwa mtihani mgumu sana kwa Joachim Loew kumuita Rudiger, Boateng, na Sane wote wakiwa wachezaji weusi. Nani angemwelewa.
Walichokosea Wajerumani ni hapa kwa Ozil. Achilia mbali macho ya Ozil yanayoonesha kuwa yeye ni mpole lakini pia anasifika kwa kuwa na moyo wa ukarimu.
Hivi majuzi Mbappe ameimbwa sana baada ya kuagiza mshahara wake wa kombe la dunia uende kwa wasiojiweza. Lakini wengine tumeshasahau kwamba Ozil alipeleka mshahara wake wote kwa watoto waliokuwa wakifanyiwa upasuaji kule Brazil. Alikuwa akipokea dola laki 2 na 40 na zote alipeleka kwa watoto wote 23.

Ozil alisema “Nimependezwa na mapokezi ya Wabrazil, ni wakarimu na wapole”
Zawadi pekee Ozil aliyoamua kuwalipa Wabrazil ni kutoa mshahara wake wote wa kutwaa ubinhwa wa kombe la dunia.
Hivi majuzi mwaka 2016, Özil alitembelea kambi ya wakambizi ijulikanayo kama Zaatari kule nchini Jordan, iliyokuwa na watu 80,000 waliopoteza makazi yao kutokana na vita vya Syria. Alitumia muda wake kucheza na watoto na kuwagawia mipira vyakula na nguo. Ni Özil huyu huyu wajerumani wanamdharau.

Mwaka 2017, akiwa na kikundi cha kusaidia wasiojiweza cha My Shining Star alimkaribisha uwanjani mtoto Charlie aliyekuwa akiugua kansa katika mchezo wao dhidi ya Sunderland katika uwanja Emirates Stadium.
Ozil ameamua kuachana na soka la timu yake ya taifa.
Mesut Ozil alikuwa mchezaji wa muhimu sana kwemye kikosi cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa dunia kule Brazil

Hata hivyo JAKE POLDEN amesema amesikitishwa na uamuzi wa Ozil lakini amesema viatu alivyovaa Ozil ni vizito kuliko safari anayotaka kusafiri.
Shida kubwa ni mchezo wao dhidi Mexico, mashabiki wengi wanadai kuwa alicheza chini ya kiwango kiasi cha kuamua kumzomea. Mchezo uliofuatwa dhidi ya Sweden kocha wake akamweka benchi Ujerumani wakashinda. Mchezo uliofuata dhidi ya Korea Kusini Ozil nae alianza ila ukilala na paka lazima uamke na mafua. Ujerumani wakapoteza tena mchezo na bado lawama zilimwendea Ozil.

Imamu Ahmed Mansour kwenye utafiti wake wa “uhuru katika Uislam” anasema kila muumini wa Kiislamu ana uhuru na haki ya kutoa mawazo yake kama alivyofanya mtume. Mtume alipokwenda Mecca na kuwa mtawala aliwaruhusu watu wote kutoa maoni na mawazo. Ozil nae kama muislam ametumia fursa hii kutoa mawazo yake. Nafsi yake inamsukuma kuamini kwamba haheshimiki na anadharauliwa. Haoni kama faifa ya Ujerumani linamtendea haki.
Ozil aliandika barua ya wazi na kusema:
“Kwa machungu moyoni na majonzi mazito baada ya kuona mambo yasioeleweka nimeamua kupumzika kuichezea Ujeruman. Sababu yangu kubwa ni ubaguzi na dharau” .
“Nimejivunia kila mara nilipovaa jezi ya timu ya taifa, lakini kwa sasa mtanisamehe. Ni maamuzi magumu sana, nimejitoa kwa ajili ya wachezaji wenzangu, makocha na viongozi wote lakini kuna mambo hayapo sawa”

“Viongozi wa juu DFB wamejisahau sana kwa kunionesha ubaguzi wa wazi kabisa kama walivyokuwa wakifanya kwa waturki wenzangy. Hii ni dharau wala siwezi kuvumilia. Wametoka nje ya mstari kisha wanaanza kuweka propaganda za kisiasa, inatosha narudia tena inatosha.
“Sichezi mpira kwa sababu za kisiasa wala sina huo muda, ubaguzi hauwezi kuvumilika na haufai.”
Ozil ametimiza umri wa miaka 29.
Akaongeza: “Sijachoka kuichezea Ujerumani lakini kauli na magendo ya viongozi wa DFB wamenifanya nisione umuhimu wa kuendelea kuvaa jezi yenye bendera la taifa la Ujerumani”
“Nimeanza kuchezea taifa hili tokea 2009 nimejitahidi sana lakini mema yangu tayari yameenda na mtaro wa maji machafu. Wameshasahau”
Barua ya Ozil, ni wazi amevumilia kwa kipindi kirefu sana. Wajerumani wenyewe wanataka kuturudisha nyuma. Ni miaka 16 tokea Wajerumani wavunje mwiko wa ubaguzi. Je wamejisahau au ni matakwa ya wachache.?
Mesut Ozil ameandika barua hii ya wazi baada ya mashabiki kumzomea. Sababu ya kumzomea kwake ni kutokana na picha aliyopiga na raisi wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan

Ozil akasema “Soka la dunia limekua sana. Tumekuwa na muingiliano mkubwa wa watu wa tamaduni na kabila tofauti. Ubaguzi haukubaliki hata kidogo katika dunia ya wapenda soka”
Ozil’ aliandika barua ya kwanza akijaribu kujitetea kitendo cha kupiga picha na raisi Recep Tayyip Erdogan back mwezi Mei picha ambayo ilimweka kwenye wakati mgumu sana.
“Kazi yangu ni kucheza soka, mimi sio mwanasiasa, mkutano wetu na Mh Raisi haukuwa na makubaliano yoyote ya kimkataba wala kisera”
Barua yake ya pili aliielekeza kwa viongozi wa DFB. Amemlaumu sana raisi wa DFB bw. Reinhard Grindel kwa kushindwa kutofautisha hisia zake za kibaguzi na soka.
“Kwenye macho ya Grindel na wafuasi wake mimi nimjerumani pale tu tunapopata ushindi lakini tunapofungwa mimi ni mzamiaji”

Raisi wa Uturuki alipigwa marufuku ya kuingia nchini Ujerumani kutokana na sababu za kisiasa.
Ozil hajaogopa hata kidogo kumsema raisi huyu wa chama cha soka cha Ujerumani. Anasisitiza watu kama Grindel hawapaswi khata kidogo kufanya kazi zinazohusiana na soka.
Ozil ameshangazwa na kwa namna baadhi ya mashabiki na viongozi walivyo unganisha ile picha na matokeo mabovu ya taifa hilo..
Baada ya kuweka barua yake ya kwanza na ya pili mashabiki wengi waliumizwa sana na tabia ya viongozi wa DFB na kumsihi Ozil awapotezee na awekeze muda wake mwingi kwa klabu yake ya Arsenal.
Wajerumani wametoka kwa aibu na fedheha kubwa. Mzigo huu wa kinyesi wakaamua kumbebesha Ozil pekee yake wakiamini kwamba dunia ya wapenda soka tutaungana nao. Baada ya Ujeruma kutolewa kombe la dunia baba yake Ozil alikerwa sana na kitendo cha mashabiki wa Ujerumani kumzomea mwanae.
“Ningekuwa mimi [Ozil]? Ningewaambia asante lakini pia nigewambia inatosha” Alisema mzee Mustafa

“Sio haki, yale ni matusi, haiwezekani hata kidogo mashabiki wako wa nyumbani wakuzomee utadhani wewe msaliti? Alianza kuzomewa hata kabla ya kombe la dunia kule Austria ni wazi walidhamiria na walikuwa na sababu za ubaguzi ndani yao”
Alisema baba yake.
Hatupaswi kumkiri Ozil kuwa mchezaji mzuri pekee ila tunapapwa kumkiri kama shujaa pekee aliyejitoa wazi wazi na kuongelea uovu wa Wajerumani wenzake. Hajamuonea mtu aibu. Ni wachache sana ambao wapo tayari kukemea maovu. Kwangu mimi Ozil ni shujaa

0 comments:

Post a Comment