Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara ameonekana
kukerwa na kitendo kilichofanywa na baadhi ya mashabiki wa Yanga
kumvamia na kumfanyia vurugu mtu mmoja aliyesadikika kuwa shabiki wa
Simba.Manara ameyaeleza hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram huku akiweka na kipande cha video kinachoonyesha tukio hilo.una aina ya watu washamba sana na hawa ndio aina ya watu
ambao tunapaswa tuwalaani..hv why baadhi ya wanayanga wanajiona wao ndio
wenye haki nchi hii peke yao?kutucharura wafanye wao ikifanya Simba ni
kosa au ushenzi wa kumpiga shabiki wetu..hv akifa huyo mtu?hili siwaachi
soon mtasikia..mapimbi kama hao mm ndio Mchungaji wao..ntawatia adabu!!
Mijitu imetoka kwenu Manyenza huko mnatuletea ujinga!! Mnavunja hadhi
ya klabu yenu na inaonekana ni klabu iliyofuga watu wahuni.
Hayo
yamekuja baada ya shabiki huyo wa Simba aliyevalia jezi ya timu hiyo
kupita kwenye jukwaa lililozoeleka kuwa la mtani wake Yanga wakati wa
mchezo wa Wanajangwani hao.
Home
»
»Unlabelled
» Video: Manara acharuka baada ya shabiki wa Simba kudundwa na mashabiki wa Yanga ‘kwahili siwaachi’
Monday, July 30, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment