Jumla ya wachezaji wanne wa timu ya vija waliyokwama kwenye mapango ya Chiang Rai nchini Thailand wamepata bahati ya kuokolewa hapo jana siku ya Jumapili kati ya wachezaji soka 12 waliyozama.
Kwa mujibu wa chombo cha Al Jazeera taarifa
za hivi karibuni zinaeekeza kuwa jumla ya wanachama nane wa klabu hiyo
ya soka ya vijana bado wamekwama kwenye mapango hayo ya kaskazini mwa
nchi ya Thailand.
Jumla
ya vijana wanne kati ya 12 waliyookolewa wamewahishwa kwenye hospitali
ya Chiang Rai, iliyopo kilomita 60 kutoka maeneo hayo kwaajili ya
matibabu zaidi.
Vijana hao wa kiume wamekwama tangu June 23 mwaka huu wakiwa walikwenda na waalimu wao kwaajili ya kutembelea mapango hayo kablaya kujaa maji.
Dunia nzima imeungana na Thailandi hii leo siku ya Jumatatu kwaajili ya kusaidia zoezi hilo kwenda kama linavyo tarajiwa huku wazazi wa watoto hao wakiendelea na maombi.

0 comments:
Post a Comment