Rais wa Liberia George Weah anamtunuku kocha wake wa zamani Arsène Wenger, na tuzo la hadhi ya juu zaidi nchini humo.
Rais
Weah, mwafrika pekee kuwai kushinda tuzo la mchezaji bora wa mwaka,
alisainiwa Wenger mwaka 1988 wakati akiwa kocha ya klabu ya Monaco.Wenger, ambaye aliondoka Arsenal kama meneja mwezi Mei baada ya miaka22 klabuni humo aliwakuza manyota kadhaa kutoka Afrika.

Wenger anaratarajiwa kuwasili mji mkuu wa Liberia Monrovia kupokea tuzo hilo siku ya Ijumaa.
Taarifa hizo zimezua maoni tofauti nchini Liberia huku wengine wakisema kuwa tuzo hiyo hastahili kupewa mtu binafsi kwa kile wamefanya kwa rais.

Wenger alikuwa kocha wa wachezaji 16 kutoka Afrika wakiwemo Kolo Toure kutoka Ivory Coast, Mlinzi raia wa Cameroon Lauren, na raia wa Nigeria Nwankwo Kanu
Rais Weah amesema kuwa Wenger "alinitunza kama mtoto wake" wakati alijiunga na Monaco, akisema kuwa "kando na Mungu, anafikiri kuwa bila ya Wenger hakuna vile nigefanikiwa Ulaya".

0 comments:
Post a Comment