Uwezo
wa kiungo mshambuliaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama umewafurahisha
mashabiki wengi wa soka, lakini Jonas Mkude amekiri kwamba mchezaji huyo
anajua sana na atakachofanya ni kujenga naye ushirikiano mzuri kwani
anaamini hawatazuilika.
Mkude
amesisitiza kwamba akisimama na Chama ndio watakuwa viungo bora zaidi
nchini. Mzambia huyo alionyesha vitu vyake wakati Simba ikitoka sare ya
kufungana bao 1-1 na Asante Kotoko ya Ghana, Jumatano iliyopita kwenye
mechi ya Simba Day.
Ufundi
mkubwa wa kupiga pasi, kumiliki mpira, kuanzisha mashambulizi lakini
pia kuituliza timu pindi inapokuwa ikishambuliwa, ndiyo sababu kubwa
ambayo imemfanya awe gumzo zaidi.
Katika
mechi hiyo ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Chama
alionekana kushirikiana vilivyo na viungo wenzake Jonas Mkude na James
Kotei katika kupanga mashambulizi na kuwatengezea nafasi za kufunga
washambuliaji, Mganda, Emmanuel Okwi pamoja na Mnyarwanda, Meddie
Kagere.
Mkude
ameliambia Spoti Xtra kuwa; “Chama ni mchezaji mzuri ambaye kila mtu
aliona uwezo wake tulipocheza na Asante Kotoko kwa hiyo binafsi sina
wasiwasi naye kwani ana kila kitu kinachohusiana na soka.”
“Naamini
kama tutacheza kwa pamoja muda mrefu na kuzoeana naamini hakuna timu
itakayokuwa na kiungo bora kama sisi, jambo kubwa ni Wanasimba wote kuwa
kitu kimoja na kuendelea kutuunga mkono, naamini kwa kufanya hivyo
msimu ujao tutafika mbali zaidi.”
0 comments:
Post a Comment