Beki Abdi Banda ameamua kumpumzisha mke wake, Zabibu Ally Kiba na sasa amerejea kazini katika kikosi cha Baroka FC.
Banda
ni Mtanzania anayekipiga katika kikosi cha Baroka FC na leo timu yake
inawafaa Cape Town City inayoongozwa na Benni MCathy, nyota wa zamani wa
Afrika ambaye sasa ni kocha.
Beki huyo wa zamani wa Coasta Union na Simba, ameiambia SALEHJEMBE kwamba alishaanza mazoezi.
“Nilimaliza
pilika za harusi, ilikuwa Dar na Tanga kama ulivyoona. Lakini ilikuwa
ni lazima kurejea kazini haraka kama ilivyotakiwa.
“Nilishaanza mazoezi na wenzangu na leo tutakuwa na mechi hiyo. Niko tayari kabisa,” alisema.
Banda amekuwa tegemeo wa kikosi hicho kinachotokea katika mji wa Polokwane nchini Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment