Thursday, August 16, 2018



Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amesema Mwandishi Silas Mbise aliyepigwa na Polisi mnamo Agosti 08 katika Uwanja wa Taifa, alimkaba na kumtishia Askari baada ya kuzuiwa kuingia sehemu aliyokuwa haruhusiwi

Mbise ambaye ni Mwandishi wa Wapo Radio alipigwa na Polisi siku hiyo ya tamasha lililoandaliwa na Klabu ya soka ya Simba maarufu “Simba Day” ambalo klabu hiyo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana.

Aidha, IGP Sirro amesisitiza kuwa Polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hilo na ulikamilika mwandishi huyo atafunguliwa mashitaka na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria

Hata hivyo, ameongeza kuwa Askari waliohusika kumpiga mwandishi huyo wanachunguzwa iwapo walitumia nguvu isiyohitajika na ikithibitika nao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi.

0 comments:

Post a Comment