Watanzania wangetamani kuona timu yao ya vijana inakwenda kucheza katika michuano mikubwa.
Safari
itaanza kwa timu hiyo ya taifa ya vijana ya Tanzania ya U17, Sereneti
Boys kucheza na Burundi katika michuano ya kuwania kufuzu kikanda Afrika
Mashariki na Kati kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho.
Michuano
hiyo inasimamiwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki (Cecafa)
na Tanzania ipo kundi, A na timu za Rwanda, Burundi na Sudan, ikiwa ni baada ya Somalia kujitoa.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari kwenye Hotel ya Peacock jijini Dar es Salaam,
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, amesema; "Tulikua na jumla ya
timu 10, lakini timu moja imejitoa ambayo ni Somalia kwa sababu
zisizojulikana, hivyo kundi A litabakiwa na timu nne, na kundi B
litabaki na timu tano vilevile, na viwanja vitakavyotumika ni viwili tu
ambavyo ni Uwanja wa Taifa, pamoja na Azam Complex.
Aidha,
katika hatua nyingine Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Cliford Ndimbo alisema kuwa “Michuano hii haitakuwa na kiingilio
na lengo kubwa ni kutoa nafasi kwa wadau wa soka kujitokeza kwa wingi,
inatoa fursa kwa 'Serengeti Boys' kujipanga na kujiandaa kama mwenyeji
wa michuano ya AFCON mwakani."
0 comments:
Post a Comment