Club ya Mbao FC ambao inajiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara chini ya kocha wake mpya Amri Said, leo Ijumaa ya August 10 2018 imetangaza jezi zake mpya.
Mbao FC ambao wameamua kuingia katika mfumo wa kisasa na kujiingizia kipato, leo wametambulisha jezi zao mpya za nyumbani na ugenini watakazotumia msimu wa 2018/19 lakini mashabiki watazipata pia madukani.
Tofauti na ilivyokuwa awali na msimu uliopita jezi za Mbao FC kwa mashabiki wataanza kuzipata madukani, hiyo ikilenga kuboresha kipato cha timu hiyo, jezi hizo wamekabidhiwa na mdhamini wao GF Trucks akipokea mwenyekiti wao Solly Njashi.
0 comments:
Post a Comment