Licha ya kuwa
na wakati mgumu ikiwemo kuyumba kwa uchumi, klabu ya Yanga imemwaga msaada wa
mipira mitatu kwa timu ya Mkamba Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la
Pili.
Msaada huo
umekabidhiwa na viongozi wa Yanga kwa Mkamba baada ya kucheza mchezo wa kirafiki
na kuweza kushinda bao 1-0 likiwekwa kimiani na Papy Tshishimbi.
Yanga
imewapa Mkamba mipira hiyo kwa lengo na madhumuni la kuwasaidia kwa ajili ya
kufanyia mazoezi ili kupigania nafasi ya kupanda daraja la kwanza.
Kikosi hicho
sasa baada ya kucheza na Mkamba kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea Dar es
Salaam kuanzia leo tayari kukipiga na USM Alger.
Yanga
itacheza na waarabu hao katika mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho
Afrika ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa jumla ya mabao 4-0 huko Algiers,
Algeria.
0 comments:
Post a Comment