Nyota
wa Manchester United, Alexis Sanchez amejikuta akifuta picha na video
zake za matangazo ambazo ameziposti muda mfupi tu tangu kufanya hivyo
baada ya kukabiliwa na maneno ya karaha, kejeli na dharau kutoka kwa
mashabiki wa United.

Sanchez leo siku ya Jumatatu aliposti picha zinazotangaza nguo zake mpya kupitia mtandao wake wa Twitter na hivyo mashabiki wa United kumjia juu kwa kumuandikia ujumbe wenye karaha, kejeli na dharau kutokana na kufanya kitendo hicho saa chache wakati klabu yake ikitoka kupokea kipigo cha mabao 3 – 2 dhidi ya Brighton mchezo wa ligi kuu England.

Mchezaji huyo wazamani wa Arsenal raia wa Chile aliposti picha na video zinazomuonyesha akiwa amevalia aina hiyo mpya za nguo zake akiwa sambamba na JJO.

Mchezaji
huyo anayelipwa zaidi ligi kuu England amejikuta akiingia kwenye matusi
ya hali ya juu kutoka kwa mashabiki ”Tumemsajili mwanamitindo
tunayemlipa 350,000 kwa wiki,” maneno ya mashabiki wa United
wakihamishia hasira ya kipigo cha ligi kuu kwa nyota huyo ambaye jana
usiku hakucheza kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

0 comments:
Post a Comment