Ligi kuu nchini Tanzania inatarajia kuanza hii leo ambapo wakati watu wakisubiri mechi ya Simba vs Prisons, kule Mwanza leo mji utasimama kwa dakika 90 kuipisha Mwanza Derby.
Ndio vinara wapya wawili wa jiji la Mwanza klabu ya Mbao Fc na Alliance Fc ambao wote wawili mdhamini wao ni mmoja kampuni ya GF Truck watakuwa pale Mwanza kuoneshana utemi.
Mchezo huu una msisimko mkubwa sana kwani hawa ni watu ambao wanajuana sana kwa kuwa karibu, lakini vile vile kuwa na mdhamini mmoja kunawafanya kuwa na kitu kimoja ambacho kinaongeza hamasa katika mchezo huu.
Shaffihdauda.co.tz ilifanikiwa kuzungumza na makocha wa timu ya Alliance na vile vile Mbao Fc kulezea maoni na mtazamo wao kuelekea mchezo wa hii leo.
Kocha wa Alliance Mbwana Makata alikuwa wa kwanza kukutana naye na alielezea machache kuelekea Derby ya leo.
“Kwenye maandalizi yetu tumecheza michezo 8 yakirafiki dhidi timu nyingine ambazo zilikuwa ni za ligi kuu (Kagera Sugar, Stand United, SingidaUnited) vijana walicheza vizuri na kushinda hizo mechi.
Nilikua najaribu mifumo mingi tofauti kwa sababu tuna wachezaji wengi kutokana na academy yetu, tumeshaona mapungufu yako wapi na tumefanyia kazi kabla ya echi yetu dhidi ya Mbao.
Tumejiandaa vilivyo kwa sababu kwenye mashindano hakuna muda cha msingi ni kuingia kwa dhamira moja kuitetea Alliance.
Tatizo lililokuwepo ni kwenye umaliziaji, tulikuwa tunatengeneza nafasi nyingi lakini hatufungi. Tumesharekebisha eneo hilo, pili tulikuwa na tatizo kwenye ulinzi pindi tunapopoteza mpira kurudi kuja kufanya coverage lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa.”
Wakati kocha wa Alliance akisema hayo, Amri Said ambaye ndiye mwalimu mpya wa Mbao Fc naye ana ya kwake kuelekea katika mchezo huo.
“Mechi yetu na Alliance naichukulia kama mechi nyingine, ni mechi ngumu kwa sababu timu zote ni za sehemu moja (derby) wachezaji wa Alliance nimewaona wanavyocheza na nimejaribu kutengeneza njia za kuzuia makali yao na kutengeneza njia za kupata pointi.
Alliance si timu ya kubeza naiheshimu na namheshimu mwalimu wao Mbwana Makata.:
Kwa 70% wachezaji wangu wanaendelea vizuri na kila kitu kipo sawa. Maboresho yamefanyika kwa kuongezea wachezaji baada ya wachezaji kama 6 kutoka kwenda kwenye vilabu vingine tumesajili vijana wengine wameanza kuzishika hizo nafasi wanaendelea vizuri kutokana na mechi za kirafiki walizocheza
0 comments:
Post a Comment