Saturday, August 18, 2018



Real Madrid waki tayari kulipa pauni milioni 270 kwa mshambualiaji wa Brazil Neymar ikiwa vikwazo vya Uefa vitawalazimisha Paris St-Germain kumuuza mchezaji huyo mwenye miaka 26. (Sport)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekana kumwinda kiungo wa kati raia wa Italia Claudio Marchisio baada ya mchezaji huo mwenye moaka 32 koondoka Juventus. (Goal)

Meneja wa Aston Villa Steve Bruce anasema Tottenham wangemsaini kiungo wa kati Muingereza Jack Grealish msimu huu ikiwa wangemueendea Mapema. (Talksport)

Mshambalizi anayeichezea Newcastle kwa mkopo raia wa venezuela mwenye miaka 28 Salomon Rondon, 28, anataka kuondoka kabisa huko West Brom. (Chronicle)

Meneja wa England Gareth Southgate atamtazama kipa wa Southampton Alex McCarthy, 28, dhidi ya Everton siku ya Jumapili wakati yuko mbioni kumtafuta kipa. (Telegraph)

Matumaini ya Tottenham ya kusaini mshambuliaji raia wa Uholanzi Vincent Janssen, 24, yamezimwa baada ya kusemekana kuwa mchezaji huyo haondoki. (Sun)

Wing'a wa Leicester Demarai Gray, 22, ameweka malengo yake ya kujiunga na kikosi cha England akisema kuwa hataki kuwatazama kutoka kwenye baa, (Sky Sports)

Meneja mpya wa West Ham Manuel Pellegrini anasema hakuna sababu kuhusu ni kwa nini wachezaji wake wanaweza kuogopa kuchezea uwanja wa London. (Guardian)

Meneja wa Everton Marcos Silva amefichua kuwa anataka wachezaji wake wote wazungumze Kiingereza kila wakati. (Telegraph)

Kutoka BBC

0 comments:

Post a Comment