Friday, January 28, 2022

 

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba leo Januari 27,2022 wamerejea salama Dar es Salaam.

Timu ya Simba chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco raia wa Hispani ilikuwa Kagera ambapo ilikuwa na mchezo wa ligi uliochezwa jana Januari 26.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 1-0 Simba na kuwafanya mabingwa hao kuyeyusha pointi tatu mazima.

Ni bao la Hamis Kiiza ambaye alikuwa akisoma mchezo akiwa benchi lilitosha kuwatuliza Simba dakika ya 70 baada ya shambulizi la kushtukizwa kufanywa na Kagera Sugar.

Francis Baraza Kocha Mkuu wa Kagera Sugar aliweka wazi kuwa waliwafuata Simba kwa tahadhari na ushindi ambao wamepata ni furaha kwao.

Simba inabaki na pointi 25 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi ya 13 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 14.

0 comments:

Post a Comment