YANGA kweli safari hii imepania kuhakikisha kuwa inawalinda mastaa wake hiyo ni baada ya uongozi wa klabu hiyo chini ya wadhamini wao, GSM kumuita fasta mshambuliaji hatari wa timu hiyo, Fiston Mayele kwa ajili ya mazungumzo.
Fiston Mayele ndani ya Yanga kwa sasa ndiye kinara wa upachikaji mabao akiwa na jumla ya mabao 6 huku akiwa wapili kwenye orodha ya wafungaji bora. Kinara wa jumla ni Reliants Lusajo wa Namungo mwenye 7.
Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumatano kuwa, uongozi wa GSM umefanya kikao na Mayele ambaye amekuwa ni msaada wa timu na hiyo ni katika kuhakikisha kuwa anaendelea kusalia ndani ya timu hiyo kwa muda mrefu zaidi.
“Ni kweli Mayele leo Jumanne (jana) alikutana na uongozi wa GSM ambao walikuwa na kikao na kubwa zaidi lilikuwa ni kuzungumza ni kwa namna gani mshambuliaji huyo anaendelea kusalia ndani ya timu kwa muda mrefu licha ya kuwa tayari ana mkataba wa miaka miwili ambao alisaini wakati anajiunga na timu hiyo.
“Unajua kuna mambo mengi kwenye mpira, unapokuwa na wachezaji wazuri lazima ufahamu jinsi ya kuishi nao na ndio maana vitu kama hivi uongozi kukaa kufanya vikao na mchezaji ni kawaida kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili yaani mchezaji na timu,” kilisema chanzo hiko.
Alipotafuta Mayele kuzungumzia juu ya ishu hiyo alisema: “Ni kweli nilikuwa na kikao na uongozi jambo ambalo sio geni kwa wachezaji na yalikuwa ni mambo binafsi ambayo nisingependa kuyaweka hadharani.
0 comments:
Post a Comment