Wednesday, August 1, 2018



Aliyekuwa beki wa Yanga, Hassan Kessy, amefanikiwa kujiunga na klabu ya Nkana Red Devils kwa kusaini mkatababwa miaka miwili.

Kessy amejiunga na klabu hiyo baada ya kushindwa kuelewana na Yanga juu ya dau la fedha ambalo alilitaka ili aongeze mkataba.

Baada ya kumalizana na Nkana, Kessy alianza mazoezi na kikosi hicho jana huko Zambia tayari kabisa kuanza safari ya maisha yake ya soka na klabu hiyo mpya.

Kessy sasa atakuwa anavaa jezi namba 22 akiwa na klabu hiyo iliyo nafasi ya 4 hivi sasa ikijikusanyia alama 45 kwenye msimu wa 2018/19.

0 comments:

Post a Comment