Moja kati ya habari zilizochukua headlines leo ni pamoja na tweet ya wakala
Dimitri Seluk kuhusiana na mteja wake
Yaya Toure raia wa
Ivory Coast,
Dimitri leo amepost ujumbe wa kuashiria
Yaya Toure anarudi uwanjani kuendelea kucheza Ligi Kuu
England katika moja ya vilabu vya juu.

Guardiola na Toure
Seluk amepost ujumbe unaoeleza hivi
“Toure
amefaulu vipimo vya afya London, Yaya anakaribia kusaini mkataba mpya,
sio wa kuichezea West Ham kwa asilimia 100 Yaya ni Bingwa” Ujumbe huo umeanza kuhusisha taarifa kuwa
Yaya atajiunga na vilabu vya
Arsenal au
Chelsea kwani ndio vilabu vikubwa vya
London.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri kocha wa
Man City Pep Guardiola alimuacha
Yaya Toure katika kikosi chake lakini staa huyo alimtuhumu
Guardiola kuwa amemuacha kwa ubaguzi wa rangi,
Seluk ambaye ni wakala wa
Toure amewahi kusikika akisema
Toure mwenye umri wa miaka 35 atabaki kucheza
EPL ili amdhiirishie
Guardiola kuwa bado ana uwezo mkubwa na alimuacha kwa chuki zake.
0 comments:
Post a Comment