Manchester City ina
wasiwasi Manchester United itawapiku katika hatua yao kumsajili
mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Ureno Ruben Neves mwenye umri wa
miaka 21 kutoka Wolves. (Goal)
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha
kati wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure,
mwenye miaka 35, anakaribia kukamilisha uhamisho wake kurudi Olympiakos.
(Mirror)Paris St-Germain wako tayari kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele wa Stoke na Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting, mwenye umri wa miaka 29. (Sun)
- Makamu rais wa zamani wa FIFA ahukumiwa kifungo cha miaka tisa
- Panya alikula sehemu ya mguu wangu nikiwa Afrika Kusini - Mabbutt
Barcelona ina imani ya kumsajili wachezaji wawili wa kiungo cha kati waliowalenga msimu ujao wa joto. Wachezaji hao ni Paul Pogba, wa manchester united na wa Paris St-Germain' raia wa Ufaransa Adrien Rabiot, na mchezaji wa kiungo cha kati wa Ajax Frenkie De Jong. (Sport)
Mchezaji anayelengwa na Barcelona De Jong anasema atasalia Ajax, lakini mchezaji huyo wa kiungo cha kati raia wa Uholanzi bado hajakataa uhamisho kwenda Nou Camp katika siku zijazo. (NOS)
Winga wa England Jason Puncheon, mwenye umri wa miaka 32, anapigwa jicho na Middlesbrough wakati Tony Pulis akitazamia kuungana upya na mchezaji huyo wa Crystal Palace. (Teesside Gazette)
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Everton raia wa Uhispania Sandro Ramirez, mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kujiunga na Real Sociedad kwa mkopo kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ijumaa. (ESPN)
Tazama pia:
- Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 29.08.2018
- Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 28.08.2018
- Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 27.08.2018
Sevilla inakaribia kumsajili winga wa Uholanzi Quincy Promes, mwenye miaka 26, kutoka Spartak Moscow katika mkataba wa thamani ya Euro milioni 20. (AS)
Mourinho ataka aheshimiwe baada ya Man United kuchwapwa 3-0 na Tottenham
Mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 23, anatarajiwa kuondoka Liverpool kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho Ulaya huku Besiktas ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyomuwania mchezaji huyo. (Liverpool Echo)

0 comments:
Post a Comment