Manchester United
inakataa kumuuza mchezaji wake wa kiungo cha kati raia wa Ufaransa Paul
Pogba, anayetaka kuhamia Barcelona. (Sun)
Arsenal ina imani
itaendelea kumzuia mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Wales Aaron
Ramsey, mwenye umri wa miaka 27, licha ya Barcelona, Lazio na ligi kuu
ya Uchina kumwinda. (Mirror)Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema anatarajiwa wachezaji wataondoka katika klabu hiyo kabla ya kufika muda wa mwisho wa uhamisho wa wachezaji Ulaya licha ya kuwa timu hiyo haikusajili mchezaji yoyote msiu huu wa joto.(Sky Sports)
Lakini mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham raia wa Ufaransa Moussa Sissoko, mwenye miaka 29, amewaambia mashabiki wake kuwa atasalia katika kalbu hiyo.(Talksport)
Chelsea imefanya mazungumzo na mchezaji wa kiungo cha mbele wa Lyon Nabil Fekir, 25, msimu wa joto lakini ikaamua kutomsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.(Goal)
Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini ametupilia mbalia hatau ya kuhama kwa mchezaji wa Ivory Coast Yaya Toure, ambaye ni ajenti wa bure baada ya kuondoka Manchester City. (Sun)
Mchezaji wa kushoto wa Manchester City Oleksandr Zinchenko huenda anakaribia kuhamishwa kwa mkopo kuelekea Real Betis au Girona baada ya mchezaji huyo wa miaka 21 kukataa ombi la kuhama kabisa kwenda Wolves msimu huu wa joto. (Mirror)
Mashabiki wa soka kuanza kuingia uwanjani Misri

Newcastle italazimika kulipa kitita cha fedha iwapo itaamua kumsajili mshambuliaji wa Venezuelan Salomon Rondon, mwenye miaka 28, katika mkataba wa kudumu msimu ujao wa joto baada ya West Brom kuidhinisha kuongeza kwa mwaka mmoja mkataba wake. (Sun)
Mshambuliaji wa Arsenal mwenye miaka 20 Stephy Mavididiis anafanya mazungumzo kuhusu mkataba wa kudumu kuelekea Juventus - baada ya kucheza kwa mkopo na Preston na Charlton msimu uliopita. (Sun)
Joao Mendes - mtoto wa gwiji wa soka wa Brazil Ronaldinho - mwenye umri wa miaka 13 alijaribu kujificha asitambulike hivi karibuni alipokuwa akifanyiwa majaribio na timu ya Brazil Cruzeiro. (Globoesporte, via Mail)
Unaweza kuvutia na hii pia:

0 comments:
Post a Comment