Sunday, August 5, 2018

Paul Pogba


Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paul Pogba
Ajenti wa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba anatarajiwa kuwaambia Red Devils kuwa anaweza kufikia makubaliano ya pauni milioni 100 kwa mshindi huyo wa kombe la dunia mwenye umri wa miaka 25 kwenda Barcelona. (Daily Star Sunday)
Pia meneja wa Manchester United Jose Mourinho anapanga kuweka siku ya mwisho kumwinda mlinzi wa England Harry Maguire, 25, ambaye amewekewa thamani ya pauni milioni 80 na Leicester. (Sunday Express)Aaron Ramsey
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Toby Alderweireld
Manchester United wanakaribia kuafikia makubaliano ya paunia milioni 60 kumsaini mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld, 29. (Sunday Mirror)
Lakini mbio za Manchester United za pauni milioni 35 kwa mlinzi wa Barcelona raia wa Colombia Yerry Mina zimefikia kikomo kwa sababu ya mvutano kuhusu malipo ya ajenti. (Sun on Sunday)
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aaron Ramsey
Chelsea wanaweka tayari pauni milioni 35 kwa kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27. (Sunday Express)
Chelsea watafanya mazungumzona mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard siku ya Jumamosi na kumpa mchezaji huyo wa miak 27 mkataba kwa pauni 300,000 kwa wiki kumzuia asijiunge na Real Madrid. (Sunday Times - subscription required)
Haki miliki ya picha Getty ImageAnthony Martials
Image caption Anthony Martial
Manchester United watamtoa mshambuliaji mfaransa Anthony Martial, 22, kwa Chelsea kumbadilisha na wing'a Mbrazil Willian, 29, huku wachezaji hoa wakiwekewa thamani ya pauni milioni 75. (Sunday Mirror)
Borussia Dortmund wanakataa kumuuza wing'a mmarekani anayewekewa thamani ya pauni milioni 60 Christian Pulisic, 19, anayetafutwa pia na Chlsea na Bayern Munich. (Mail on Sunday)
Wolves wametoa ofa ya pauni milioni 16 kwa mlinzi wa Besiktas na Croatia Domagoj Vida, 29. (Sabah - in Turkish)
Haki miliki ya picha Getty ImagesJose Mourinho
Image caption Jose Mourinho
Jose Mourinho atakuwa meneja wa Ureno ikiwa ataondoka Manchester United. (Sunday Mirror)
Benfica wameanzisha mazungumzo kumsaini beki wa Manchester United na Italia Matteo Darmian ambaye amewekewa thamani ya pauni milioni 15m. (Sun on Sunday)
Leicester wanakaribia kumsaini wing'a wa Algeria Rachid Ghezzal, 26, kutoka Monaco. Mchezaji hyo amekuwa akiwindwa na Watford na Southampton. (ESPN)
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lucas Perez
Lucas Perez
Arsenal wamekubali ofa ya pauni milioni 4.45 kutoka kwa Sporting Lisbon kwa mshambuliaji wa Uhispania Lucas Perez, 29. (A Bola - in Portuguese)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Ublegiji Mousa Dembele, 31, amekaa kuelekea Inter Milan. (Sun on Sunday)
Fulham wameuliza kuhusu kumsaini beki Real Madrid mfaransa Theo Hernandez, 20, kwa mkopo. (Mail on Sunday)

0 comments:

Post a Comment