Mwandishi wa Habari za Michezo kutoka Kigali, Rwanda, Clever Kazungu, amefunguka kwa kuthibitisha kuwa kiungo Haruna Niyonzima ameanza safari ya kuelekea Tanzania.
Kazungu ameeleza kuwa mchezaji huyo jana ameagana na uongozi wa AS Kigali aliyokuwa akiichezea na akigawa jezi yake namba nane kwa mchezaji mwingine.
"Niyonzima jana ameaga kwa mabosi wake na inaonekana tayari atakuwa ameanza safari ya kuelekea Tanzania.
"Kinachosubiriwa hivi sasa ni yeye kuwasili tu Dar es Salaam kwa maana hata jezi yake ameshaigawa kwa mchezaji mwingine."
0 comments:
Post a Comment