Wednesday, August 22, 2018


Wachezaji wanne wa timu ya taifa ya Japan ya mpira wa kikapu waliyokuwa kwenye michuano ya Asian Games wamerudishwa nyumbani baada ya kuripotiwa kufanya mapenzi na watoto wa kike.

Kwa mujibu wa tovuti ya KYODO NEWS inaeleza kuwa  wachezaji hao walitoroka kambini na ‘ uniforms’ mara baada ya mchezo wao dhidi ya Qatar siku ya Alhamisi na kuaga kuwa wanakwenda kupata chakula kisha kutoroka na kwenda kwenye hoteli ya Jakarta ambapo waliweza kulala na watoto hao wa kike mpaka asubuhi ya Ijumaa.

Wakati wachezaji hao wakiwa ni Takuya Hashimoto, Keita Imamura, Yuya Nagayoshi pamoja na Takuma Sato. Kamati ya michuano ya Olympic nchini Japan ndiyo iliyoamua vijana hao kurudishwa nyumbani mapema kufuatia tuhuma hizo.

Japan, ambayo imeshinda taji hilo miaka minne iliyopita imeipiga timu ya Qatar 82-71 katika mchezo wao wa pili uliyopigwa Jakarta na kuwafanya kuwa vinara wa Group C.

0 comments:

Post a Comment