Vijana
wa Tanzania, Serengeti Boys watacheza kuwania mshindi wa tatu katika
michuano ya Kombe la Cecafa chini ya miaka 17 baada ya kukubali kipigo
cha mabao 3-1 kutoka kwa Uganda.
Uganda
ambao wamekuwa wakilalamikiwa na makocha kadhaa kuwa na wachezaji
vijeba, wameifunga Serengeti Boys kwa mabao hayo 3-1 kwenye mchezo wa
nusu fainali kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Katika
mchezo huo, mabao ya Uganda yalifungwa na Abdulwahid Iddi, John Alou na
la tatu Alphonce Msanda akajifunga huku lile la kufutia machozi la
Serengeti Boys lilifungwa na Edson Mshirakandi aliyechonga kona moja kwa
moja.
Kwa
ushindi huo, Uganda watawavaa Ethiopia katika mechi ya fainali huku
Serengeti Boys wakissubiri kucheza kuwania mshindi wa tatu dhidi ya
Rwanda waliofungwa kwa penalti 4-2 na Ethiopia baada ya sare ya 2-2
katika muda wa kawaida.

0 comments:
Post a Comment