Muda unakwenda mbio: Tarehe ya mwisho ya wachezaji kuhama ni Alhamisi hii itashuhudia vilabu vikinga'ng'ana kufikia mikataba.Je Tottenham hatimaye watamsaini mchezaji? Anthony Martial atabaki Manchester United?
BBC inaangazia wachezji watano ambao huenda wangafunganya virago kabla ya tarehe ya mwisho.
Toby Alderweireld (Tottenham)
Haki miliki ya pichaGetty Images
Image caption
Toby Alderweireld
Nafasi: Mlinzi
Miaka: 29
2017-18 Mechi za Ligi ya Premier: 15
Amehusiswa na: Manchester United
Mlinzi huyu Mbelgiji Alderweireld alikuwa na
wakati mgumu kudumisha nafasi yake huko Tottenham baada ya jeraha
kumweka nje msimu uliopita.
Mkataba wa Alderweireld unaisha
mwisho wa msimu na kutokana na kuwa Manchester United wanammezea mate
bei aliyowekewa ya pauni milioni 75 itakuwa kizuizi.
Jack Grealish (Aston Villa)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Jack Grealish (Aston Villa)
Nafasi: Kiungo wa kati
Umri: 22
2017-18 Mechi za Championship League: 30, mabao 3
Amehusishwa na: Tottenham, Chelsea
Mchezaji wa England wa kikosi cha wachezaji wa
chini ya miaka 21 alifanya vizuri wakati Villa walikuwa waking'ang'ania
ubingwa ambapo walishindwa na Fulham.
Aston Villa wana matatizo ya
kifedha na Grealish amewavutia Tottenham ambao wanataka kumsaini kwa
pauni milioni 20 lakini meneja Steve Bruce anahitaji mara mbili pesa
hizo.
Danny Ings (Liverpool)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Danny Ings (Liverpool)
Mshambuliaji huyu wa England amepitia misimu
mitatu smigumu huko Anfield na kafunga tu bao moja wakati wa mechi za
Ligi ya Primia msimu uliopita.
Hilo hata hivyo halijawazuia the
Reds kumwekea bei ya pauni milioni 20 mchezaji huyo huku ripoti zikisema
kuwa Crystal Palace huenda wakamsaini.
Harry Maguire (Leicester)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Harry Maguire (Leicester)
Nafasi: Mlinzi
Umri: 25
2017-18 Mechi za Premier League: 38, mabao 2
Amehusishwa na: Manchester United
Beki huyu amekuwa tegemeo kubwa kwa klabu yake na pia timu ya taifa.
Jose
Mourinho anamwinda kwa mkataba wa pauani milioni 65 licha ya Leicester
nao kutajwa kumwinda kwa pauni milioni 80 ambayo itakuwa ni rekodi ya
dunia kwa mlinzi.
Anthony Martial (Manchester United)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Anthony Martial (Manchester United)
Nafasi: Wing'a
Umri: 22
2017-18 Mechi za Premier League: 30 mabao 9
Amehusishwa na: Tottenham, Chelsea, Paris St-Germain
Martial amekuwa na wakati mgumu kuwa katika
kikosi cha kwanza tangu Alexis Sanchez awasili na alikosa nafasi katika
kikosi cha Ufaransa kilichoshinda kombe la dunia.
Mourinho
hakufurahishwa baada Martial kuondoka kwenye safari ya Marekani ya mechi
za maandalizi na kurudi Ufarana kuwepo wakati wake anajifungua mtoto wa
pili na anatarajai kumuuza pauni milioni 80.
Simon Mignolet (Liverpool)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Simon Mignolet (Liverpool)
Nafasi: Mlinda Lango
Umri: 30
2017-18 Mechi za Premier League: 10
Amehusishwa na: Barcelona, Besiktas
Kipa huyu mbelgiji alikuwa namba mbili kwa
Karius lakini ameshuka zaidi baada ya kuwasili kwa raia wa Brazil
Alisson kutoka Roma.
La kushangaza ni kuwa mabingwa wa La Liga
Barcelona wanataka kumfanya Mignolet namba mbili baada ya Marc-Andre Ter
Stegen, , huku Besiktas wakimmezea mate wanapomtafuta kipa mpya baada
ya kumuuza Fabri kwenda Faulham
Aaron Ramsey (Arsenal)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Aaron Ramsey (Arsenal)
Nafasi: Safu ya kati
Umri: 27
2017-18 Mechi za Premier League: 24, mabao 7
Amehusishwa na: Chelsea, Liverpool
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Wales Ramsey
amemaliza msimu 10 huko Arsenal akicheza zaidi ya mechi 300 lakini
huenda akakumbwa na changamoto mpya kwenye mwaka misho mkataba wake.
Meneja
mpya Unai Emery alimtajaa Ramsey kama mchezaji muhimu lakini mahasimu
Chelsea wanaripotiwa kujipanga na pauni milioni 35 na hata Liverpool.
Willian (Chelsea)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Willian (Chelsea)
Nafasi: Wing'a
Umri: 29
2017-18 Mechi za Premier League: 36, mabao 6
Amehusishwa na: Barcelona, Real Madrid, Manchester United
Wing'a mwenye bidii alicheza kwenye mechi zote za kombe la dunia za Brazil
Willian
alikosa mazoezi ya msimu mpya kutokana na tatizo kwenye na pasipoti
yake na anaweza kuelekea Real Madrid kwa pauni milioni 65.
Wilfried Zaha (Crystal Palace)
Haki miliki ya pichaGetty ImagesImage caption
Wilfried Zaha (Crystal Palace)
Nafasi: Wing'a
Umri: 25
2017-18 Mechi za Premier League : 29, mabao 9
Amehusishwa na: Borussia Dortmund, Chelsea, Tottenham
Licha ya kutocheza wiki tano za kwanza msimu uliopita Zaha aliwafungia palace bao 9.
Meneja
Roy Hodgson anasema anataka raia huyo wa Ivory Coast kubaki lakini pesa
nyingi zinaweza kuwaweka kwenye majaribio ya kumuuza.
0 comments:
Post a Comment